Othman akomaa na ahadi ya kuimarisha demokrasia
Unguja. Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Othman Masoud Othman, amesema endapo akishika madaraka Oktoba 29, mwaka huu atahakikisha anajenga demokrasia ili Wazanzibari wawe huru kuchagua na kuchaguliwa katika chaguzi huru. Amefafanua kuwa Serikali atakayoiunda itakomesha utaratibu wa viongozi kuchaguliwa kwa njia zisizo halali, hali inayosababisha Wazanzibari kupokwa haki yao ya kuchagua…