Admin

DC Mpogolo azindua vitabu kwenye MwanaClick

Dar es Salaam. Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amesema utunzi wa vitabu unaofanywa na watu mbalimbali nchini ni ushahidi wa wazi wa mapinduzi chanya ambayo Tanzania imeyapitia katika nyanja mbalimbali za maendeleo. Mpogolo amesema kuwa kitendo cha Watanzania kujitokeza kuandika na kuchapisha vitabu ni ishara ya jamii inayozidi kukomaa kielimu, kiutamaduni na kitaaluma,…

Read More

Mtandao mpya wa kuwatafutia wabunifu mitaji wazinduliwa

Dar es Salaam. Wamiliki wa kampuni changa za kibunifu (Startups) huenda wakawa mbioni kuondokana na changamoto ya mitaji baada ya kuzinduliwa mtandao utakaowaunganisha na wawekezaji. Uzinduzi wa mtandao huo umefanyika wakati ambao mtaji ni kilio kwa wabunifu, hali inayosababisha mawazo yao kushindwa kuendelea na kuleta tija iliyokusudiwa kwa jamii. Mtandao ujulikanao Malaika (Rhapta Angels Investor…

Read More

Zitto azindua kampeni akiahidi kurejesha heshima ya Kigoma

Kigoma/Dar. Uwanja wa Mwami Ruyagwa, mjini Kigoma umegeuka bahari ya zambarau, umati uliovaa vazi la rangi hiyo ulipofika kushuhudia uzinduzi wa kampeni za mgombea ubunge wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe. Zitto, kiongozi mstaafu wa chama hicho amesema leo Septemba 6, 2025 kuwa safari yake ya kisiasa iliyoanza mwaka 2015 na kukwama 2020 sasa itaendelea kwa nguvu…

Read More

BALOZI NCHIMBI AKIWASILI KATIKA JIMBO LA BIHARAMULO MAGHARIBI

Mgombea Mwenza wa Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akiwasili katika uwanja wa mpira CCM Majengo,katika jimbo la Biharamulo Magharibi mkoa wa Kagera,ambapo baadae atawatubia Wananchi waliofika kumsikiliza leo Jumamosi Septemba 6,2025 akitokea mkoa wa Kagera. Dkt Nchimbi anaendelea na mikutano yake ya kampeni nchi nzima, kusaka kura za ushindi…

Read More

Makada 18 wa Chadema washikiliwa na polisi

Moshi. Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro linawashikiliwa watuhumiwa 18, akiwamo Katibu Mwenezi wa Baraza la Vijana Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Felius Kinimi, wakituhumiwa kufanya mikusanyiko iliyo kinyume cha sheria. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao leo Septemba 6, 2025, akisema wamekamatwa eneo la…

Read More

KUPATWA KWA MWEZI KESHO SEPT 7

…………….. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa taarifa ya tukio la kupatwa kwa Mwezi linalotarajiwa kutokea kesho tarehe 7 Septemba 2025. Kwa mujibu wa Taarifa hiyo imeeleza kuwa Hali ya kupatwa kwa Mwezi ni tukio linalotokea wakati Dunia inapita kati ya Jua na Mwezi na kusababisha kivuli cha Dunia kuwa katika uso wa…

Read More

Ahadi Katiba mpya zawaibua Warioba, wanasheria nguli

Dar es Salaam. Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Jo-seph Warioba amesema licha ya ahadi za kuvutia kuhusu uanzishwaji wa mchakato wa Katiba mpya, nyuma ya kauli hizo kuna kikwazo cha utashi wa kisiasa kinachodhoofisha upatikanaji wake. Amesema kutokana na kikwazo hicho mara nyingi tume na taasisi zinazoundwa kuhusiana na suala hilo, huegemea zaidi katika masilahi binafsi…

Read More

Wananchi wamtwisha kero Nchimbi wakitaka halmashauri ya Katoro, aahidi hospitali mpya

Chato. Wakati Chama cha Mapinduzi (CCM), ikiahidi miradi mbalimbali Mkoa wa Geita, wananchi wa Katoro wametaka Halmashauri ya Geita Vijijini igawanywe ili kuwapunguzia adha ya kutembelea zaidi ya kilomita 80 kufuata huduma. Novemba 4, 2019, Halmashauri ya Geita ilihamia Kata ya Nzera iliyopo Jimbo la Geita Vijijini. Wananchi wanataka igawanywe iwe Halmashauri ya Geita na…

Read More

BENDERA ZA CHADEMA ZIKIPEPEA KWA MADAHA KUFURAHIA KAMPENI ZA MGOMBEA URAIS CCM…

Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Njombe KUNA mambo yanaleta raha Kiasi kwamba hata wale ambao hawana nafasi ya kuzungumza basi hutumia mbinu mbalimbali kufikisha ujumbe kwa jamii inayozunguka Leo Septemba 6,2025 wakati wa mkutano wa kampeni za mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) ukifanyika katika Jimbo la Makambako mkooni Njombe pamoja na kuwepo na mabango mbalimbali yaliyokuwa…

Read More