
Chadema Morogoro mjini wapata viongozi wapya
Morogoro. Baada ya vuta nikuvute ya uchaguzi viongozi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Morogoro mjini, hatimaye chama hicho kimepata viongozi wapya wa jimbo na mabaraza watakaoongoza kwa kipindi cha miaka mitano. Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo leo Juni Mosi, 2024, msimamizi wa uchaguzi ambaye pia ni mjumbe wa kamati kuu na operesheni kamanda…