
Bodi ya mfuko wa barabara yakusanya mapato asilimia 77.
Bodi ya Mfuko wa Barabara imekusanya mapato kwa asilimia 77 ya mapato yote ya bajeti ya mwaka 2023/24. Haya yamebainishwa bungeni na Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa wakati wa kuwasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2024/25. Amesema katika mwaka wa fedha 2023/24, Bodi ilipanga kukusanya Shilingi bilioni 856.795 na kati ya fedha hizo,…