
Sugu ambwaga Msigwa uenyekiti Chadema Kanda ya Nyasa
Njombe. Aliyekuwa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, maarufu Sugu ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kanda ya Nyasa akimbwaga mpinzani wake Mchungaji Peter Msigwa. Sugu amemshinda Msigwa ambaye alikuwa anatetea nafasi yake kwa kura 54 kwa 52 na sasa kada huyo ataiongoza kanda hiyo kwa miaka mitano…