
Wataka elimu ya afya ya akili itolewe shuleni
Dar es Salaam. Wakati matukio ya watu kujiua yakiendelea kushika kasi nchini yakiwahusisha watoto na vijana, wito umetolewa kwa kuwepo mkakati utakaowezesha elimu ya afya ya akili kujumuishwa kwenye mitaala ya elimu sambamba na huduma za unasihi kutolewa shuleni. Hatua hii itawezesha kuwasaidia wanafunzi kujua njia sahihi za kukabiliana na changamoto zao hasa zinazowaathiri kisaikolojia….