Bondia Mkojani apokewa kwa mbwembwe Zanzibar akirudi na medali
KATIBU Mtendaji Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar, Said Kassim Marine, amesema milango ya mchezo wa masumbwi visiwani hapa imefunguka kimataifa, hivyo wanamichezo wanapaswa kuitumia fursa hiyo ipasavyo. Ameyasema hayo jana Oktoba 23, 2025 wakati wa kuwapokea mabondia, Ali Mkojani na Suleiman Mtumwa. Mabondia hao walikwenda Brazil kushindana ambapo Mkojani amerejea na medali ya shaba…