Aliyekuwa Waziri Mkuu Thailand kutupwa jela mwaka mmoja
Bangkok. Mahakama Kuu ya Thailand imeamuru waziri mkuu wa zamani, Thaksin Shinawatra, kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela, baada ya kubaini hakutimiza ipasavyo kifungo chake cha awali alichotumia muda mwingi hospitalini badala ya gerezani. Katika uamuzi uliosomwa juzi Jumatatu, majaji walisema Thaksin, mwenye umri wa miaka 76, alihamishiwa hospitalini kinyume cha sheria wakati akianza kutumikia…