
NBC yakabidhi Kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC, yaahidi maboresha zaidi
Mdhamini mkuu wa Ligi Kuu ya NBC (NBC Premiere League), Benki ya NBC, imekabidhi kombe la ubingwa wa ligi hiyo kwa timu ya Yanga SC ya jijini Dar es Salaam huku ikiahidi kuendelea kufanya maboresho makubwa kwenye ligi hiyo katika kipindi cha miaka minne iliyosalia ya utekelezaji wa mkataba wa udhamini huo. Anaripoti Mwandishi Wetu…