
TANROADS YAANZA UTEKELEZAJI MAAGIZO YA WAZIRI BASHUNGWA//YATANGAZA ZABUNI UJENZI MADARAJA YA CHAKWALE NA NGUYAMI
Wakala ya barabara Tanzania (TANROADS) umeanza kutekeleza maagizo ya Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa aliyoyatoa Februari 22, 2024 wakati wa ziara yake ya siku Nne Mkoani Morogoro ya kukagua miundombinu ya Barabara ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kumtaka Waziri huyo kufika kusiko fikika ili kutatua kero za wananchi…