
Lissu akabidhiwa gari lake lililoshambuliwa kwa risasi
Dar es Salaam. Makamu Mwenyekiti Chadema-Bara, Tundu Lissu amekabidhiwa gari lake aina ya Toyota Land Cruiser V8, VXR na Jeshi la Polisi, jijini Dodoma, ikiwa ni takriban miaka saba tangu aliposhambuliwa. Gari hilo alilokabidhiwa leo, Mei 17, 2024 lilikuwa limehifadhiwa katika yadi ya Kituo Kikuu cha Polisi Dodoma tangu Septemba 7, 2017 aliposhambuliwa kwa risasi…