
Ukisambaza picha za ajali Mbeya kukiona cha moto
Mbeya. Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mbeya, linakusudia kutumia sheria dhidi ya wananchi wanaokimbilia kupiga picha za matukio ya ajali na kusambaza kwenye mitandao ya kijamii, jambo linalozua taharuki katika jamii. Hatua hiyo imekuja kufuatia tabia ya baadhi ya wananchi kuanza kupiga picha na kuzisambaza mitandaoni pindi ajali zinapotokea, badala ya kusaidia uokoaji…