Admin

Uzembe watajwa chanzo cha ajali iliyoua saba Morogoro

Morogoro. Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani hapa, Alex Mkama amesema chanzo cha ajali iliyoua watu saba mkoani hapa ni  uzembe wa dereva wa lori aliyetaka kuyapita magari yaliyokuwa mbele yake bila kuchukua tahadhari.  Ajali hiyo imetokea leo Jumanne Mei 14, 2024 asubuhi Dakawa Wilaya ya Mvomero ikihusisha lori na gari ndogo aina ya Toyota…

Read More

Wizara yaombwa kuchunguza ubora wa maabara za udongo

Geita. Wizara ya Madini imeombwa kuchunguza ubora wa maabara za sampuli za udongo unaosadikiwa kuwa na dhahabu kutokana na baadhi  kutoa majibu yasiyoendana na uhalisia, hivyo kuwasababishia wachimbaji hasara ya mamilioni ya fedha.  Pia, imeombwa kuwafungia watu wanaojitambulisha kuwa ni wajiolojia na kupewa maeneo ya kutafiti kisha kutoa majibu ya uongo huku wakijipatia fedha kwa…

Read More

Benki ya NBC Yaitambulisha Rasmi ‘NBC Connect’ Zanzibar

Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imetambulisha rasmi huduma yake ya kidigitali ya ‘NBC Connect’ Visiwani Zanzibar. Huduma hiyo ya kisasa mahususi kwa makampuni pamoja na taasisi mbalimbali huwezesha huduma salama na haraka za kibenki kwa njia ya mtandao ikiwa ni muitikio wa benki hiyo katika kuunga mkono jitihada za serikali za kuongeza ujumuifu katika…

Read More

WAZIRI MKUU AKUTANA NA MKURUGENZI MKAZI WA UNICEF

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo Mei 14, 2024 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto(UNICEF) Elke Wisch, Ofisini kwa Waziri Mkuu Bungeni Jijini Dodoma. Katika mazungumzo yao Mheshimiwa Waziri Mkuu amemuahidi Bi. Wisch kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kulipa ushirikiano Shirika hilo ili liweze kutekeleza majukumu…

Read More

Samia ataja changamoto upatikanaji nishati safi Afrika

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan ametaja changamoto tatu zinazokwamisha upatikanaji wa nishati safi ya kupikia, ikiwamo gharama kubwa za vyanzo vya nishati. Changamoto nyingine ni mataifa tajiri kutotoa kipaumbele kwa upatikanaji wa nishati safi ya kupikia na kutoshirikishwa kwa wadau wakiwamo wa teknolojia za kuzalisha nishati hiyo. Rais Samia ambaye ni mwenyekiti mwenza…

Read More

PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI YA RAIS SAMIA NCHINI UFARANSA.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Waziri anaeshughulikia Masuala ya Maendeleo ya Kimataifa wa Ufaransa Mhe. Chrysoula Zacharopoulou walipokutana Jijini Paris Ufaransa tarehe 13 Mei, 2024.  Rais Samia yupo nchini Ufaransa kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa Nishati Safi ya Kupikia kwa Afrika…

Read More

WEKEZA KATIKA UTAFITI KUCHOCHEA MAENDELEO: DKT. BITEKO

Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa Serikali inatambua umuhimu na mchango wa utafiti wa kisayansi katika nyanja za kijamii, kiuchumi na kisayansi zinazochangia kuchochea maendeleo ya nchi. Dkt. Biteko ameyasema hayo leo Mei 14, 2024 jijini Dar es…

Read More