Admin

Ouma anavyoibeba Coastal Union Ligi Kuu

KOCHA Mkuu wa Coastal Union, David Ouma amefanikiwa zaidi kutengeneza timu kimbinu na kiufundi, akijitahidi kumfanya kila mchezaji kuwa bora katika nafasi yake. Kocha huyo ambaye alianza kuifundisha Coastal Union, Novemba 9, mwaka jana akichukua mikoba ya Mwinyi Zahera ambaye alishindwa kuendana na kasi ya timu hiyo tayari ameanza kuandika rekodi zake ndani ya kikosi…

Read More

Askari Kinapa, mgambo matatani wakituhumiwa kwa mauaji

Moshi. Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, linawashikilia askari wawili wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (Kinapa) na mgambo kwa tuhuma za kumuua kwa risasi kijana Octovania Temba. Temba ni mkazi wa Kijiji cha Komela kilichopo Kata ya Marangu Magharibi, wilayani Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro. Wakazi wa Kijiji cha Komela kilichopo Kata ya Marangu Magharibi, wilayani…

Read More

Dabo anazitaka 12 Azam FC

MATARAJIO ya Azam FC kwa sasa ni kukusanya pointi 12 katika mechi nne zilizosalia za Ligi Kuu Bara huku ikiiombea Simba iteleze kidogo tu ili wao wasiikose nafasi ya pili itakayowafanya washiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao. Hesabu hizo za Azam zinaonekana kuwa ngumu kidogo lakini wenyewe wana matumaini hayo licha ya…

Read More

Trafiki kuvishwa majaketi yenye kamera kudhibiti rushwa

Dodoma. Serikali imesema iko kwenye mchakato wa kutumia majeketi yenye kamera watakayovaa askari wa usalama barabarani ‘trafiki’ kama sehemu ya kifaa cha kazi kwa lengo la kudhibiti rushwa barabarani. Hayo yamesema leo Jumamosi Mei 5, 2024 na Makamu wa Rais Dk Philip Mpango wakati akifungua Kituo cha Polisi Daraja A Wilaya ya Kipolisi Mtumba jijini…

Read More

Vita nane mpya ligi kuu

NDANI ya Ligi Kuu Bara achana na nani anataka kuwa bingwa, kuna vita fulani zinachukua nafasi taratibu nje na kuwania taji la ubingwa. Zitazame vita nane ambazo zinapatikana kivyake kwenye msimu huu wa ligi hiyo ukiwa unaelekea ukingoni ambazo zimekuwa zikizalisha ushindani mwingine. Simba kamchapa Azam juzi kwa mabao 3-0 ukiwa ni mchezo ambao ulikuwa…

Read More

Hatima ya Zuma kuwania urais Afrika Kusini yasubiri Mahakama

Afrika Kusini/ AFP. Mahakama ya Juu nchini Afrika Kusini imeanza kusikiliza rufaa kuhusu iwapo Rais wa zamani, Jacob Zuma atastahili kugombea tena nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu ujao. Zuma (82) anaongoza chama kipya cha upinzani, Umkhonto we Sizwe (MK), ambacho wachambuzi wanasema kinaweza kuwa na athari kubwa kwenye matokeo ya uchaguzi mkuu wa Mei 29,…

Read More

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa wingi kura za azimio linalounga mkono Palestina kuwa mwanachama kamili wa umoja huo. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa… (endelea). Azimio hilo limeitambua Palestina kuwa na hadhi ya kupata uanachama kamili na linatoa mwito kwa Baraza la  Usalama la Umoja wa Mataifa kuunga mkono azma ya Palestina…

Read More