
Wapalestina waukimbia mji wa Rafah – DW – 08.05.2024
Licha ya mayowe kutoka kwa jamii ya kimataifa kupinga mashambulio hayo ya ardhini, Israel ilipeleka vifaru vyake katika mji wa Rafah hapo jana Jumanne na wanajeshi wake wakakiteka kivuko kinachounganisha mji wa Rafah na Misri ambacho ni njia kuu ya kupitishia misaada kwenda katika eneo lililozingirwa la Palestina. Soma Pia: Guterres asema kushambulia Rafah itakuwa janga…