
Shekilango alivyofariki katikati ya misheni maalumu Uganda
Dar es Saalam. Miaka 44 imetimia tangu kufariki kwa kiongozi Mtanzania, Hussein Shekilango ambaye barabara maarufu ya Shekilango ilipewa jina hilo kwa heshima yake. Ilikuwa Jumapili ya Mei 11, 1980, Tanzania ilipompoteza waziri wake, Shekilango katika ajali ya ndege iliyotokea Arusha. Shekilango alikuwa Meneja Mkuu wa Shirika la Usagishaji la Taifa (NMC) kabla ya kuchaguliwa…