
Kibu D, namba na hali halisi vinapotofautiana
SIJUI kama tutajua tufuate lipi katika soka la kisasa. Takwimu au macho yetu? Tangu tuanze kushika kompyuta zetu soka limeanza kutuchanganya. Tuamini katika lipi kati ya tunachokiona kwa macho au takwimu. Wiki iliyopita ilikuwa ya Kibu Dennis. Sijajua ukweli hadi sasa. Tulichosikia ni hajataka kusaini mkataba mpya pale Msimbazi na anataka kuondoka zake pindi msimu…