
MTU WA MPIRA: Kwanini Mgunda asiaminiwe moja kwa moja?
MLETE MGUNDA. Ni kauli maarufu zaidi kwa wapenzi wa Simba pale mambo yanapokuwa magumu kwao. Kwanini? Subiri nitakwambia. Hapa majuzi aliyekuwa kocha wa Simba, Abdelhak Benchikha aliomba kuondoka klabuni hapo kutokana na matatizo ya kifamilia. Ilikuwa ni mshtuko mkubwa sana. Simba ilishaweka matumaini makubwa kwa Benchikha kusuka timu ya msimu ujao. Benchikha hakua na msimu…