
Mwafaka mgomo wa daladala Tanga – Horohoro Jumatatu
Tanga. Madereva wa mabasi madogo yanayofanya safari zake kati ya Tanga mjini na Horohoro Wilaya ya Mkinga waliogoma jana Mei 2, 2024 kusafirisha abiria, leo Ijumaa Mei 3, 2024 wameendelea na kazi kwa makubaliano ya kutoza Sh3, 500 hadi Jumatatu, pande tatu zitakapokaa kujadiliana. Madereva hao walikuwa wanapinga uamuzi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini…