
Unyanyapaa kikwazo mabinti waliojifungua kurejea shuleni
Dar es Salaam. Licha ya Serikali kuruhusu wanafunzi waliokatisha masomo kwa ujauzito kurejea shuleni baada ya kujifungua, utafiti umeonyesha wengi wanashindwa kuendelea na masomo kwa sababu mbalimbali, ikiwemo unyanyapaa. Ripoti ya utafiti uliofanywa na Shirika la Hakielimu katika wilaya 12 za mikoa sita nchini iliyotolewa Aprili 29, 2024 inaonyesha kwa kiasi kikubwa unyanyapaa unafanywa na…