
SMZ yatenga Sh34 bilioni posho ya nauli kwa wafanyakazi
Unguja. Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Zanzibar (Zatuc), limewasilisha changamoto nane mbele ya Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi likiomba kufanyiwa kazi ili kuongeza ufanisi kwa wafanyakazi. Wakati Zatuc ikiwasilisha changamoto hizo, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imetenga Sh34 bilioni kwa ajili ya posho ya nauli kwa wafanyakazi, kila mtumishi atapewa Sh50,000. Akisoma risala…