
PATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO APRILI 26,2024
Home » PATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO APRILI 26,2024 About the author
Home » PATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO APRILI 26,2024 About the author
Dar es Salaam. Utafiti umebaini asilimia 79 ya wanasiasa wanawake wanaotumia mitandao ya kijamii nchini Tanzania walidhalilishwa kwa kufanyiwa ukatili wa kijinsia wa aina mbalimbali kupitia mitandao yao ya kijamii. Udhalilishaji huo ni pamoja na ukiukwaji wa faragha za mtu, kuchafua sifa ya mtu, vitisho na vurugu za moja kwa moja, maneno na lugha ya…
Na Mwandishi WetuBARAZA la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET), Kanda ya Magharibi, limewapatia elimu wanafunzi 5,000 katika shule za sekondari 20 za Manispaa ya Tabora kuhusu kazi za Baraza, taratibu na miongozo mbalimbali ya kujiunga na vyuo vya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi nchini. Akizungumza na…
Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika maeneo mengi nchini zinatarajiwa kukoma Aprili 28, 2024. TMA imesema mifumo inayosababisha viashiria vya mvua kubwa inaenda kudhoofu. Meneja wa Utabiri wa TMA, Dk Mafuru Kantamla amesema hadi kufikia Aprili 28, 2024 mifumo inaonyesha hali ya mvua kubwa itakoma….
NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limetoa elimu ya viwango vya ubora kwa Wajasiriamali wadogo waliojitikeza katika Maonesho ya Kibiashara ya Miaka 60 ya Muungano katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam. Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo leo Aprili 25,2024, Afisa Masoko (TBS), Bw. Mussa Luhombero amesema wametoa elimu…
Geita. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kuwa hatima ya maisha ya Watanzania ipo kwenye mikono, mioyo na akili zao. Amesema kila kona ya nchi kuna malalamiko bila kujali aina ya shughuli wanazofanya na kusema, utafiti uliofanywa na chama hicho umebaini malalamiko na matatizo mengi ya wananchi yanatokana na mfumo wa utawala unaotokana na Katiba…
-95.28% kuelekezwa kwenye maendeleo-Serikali kuja na Kanuni ya Uwajibikaji kwa wananchi Miradi ya Mafuta na Gesi Asilia-Dkt. Biteko aagiza Halmashauri kupeleka fedha za Ushuru wa Huduma vijijini-Masharti ufunguzi wa vituo vya CNG yarekebishwa kuvutia uwekezaji-Kapinga atilia mkazo utekelezaji Nishati Safi ya Kupikia na CNG Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo limepitisha shilingi Trilioni…
KAMA ilivyo kwa wazazi, huwa na mipango yao juu ya watoto wao, bila kujua kuwa baadae inaweza isitimie ndivyo ilivyotokea kwa Mzee Abdallah Hamad ‘Bacca’. Kuna wakati unamwacha mtoto au mtu wako wa karibu kufanya kile anachokipenda zaidi hata kama wewe hukipendi kwa sababu yeye ndie anayekifanya. Lakini tunaambiwa ni bora kumwacha mtu afanye anachokipenda…
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameipongeza Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kwa kazi kubwa waliyoifanya kuwaletea maendeleo wanawake na kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na kuandaa mdahalo wa wanawake na Muungano. Pia, ameupongeza umoja huo kwa kuendelea kuwa kinara katika kubuni na kutengeneza…
Dar/mikoani. Ni wimbi la majanga lililopoka uhai wa binadamu, kuathiri makazi na hata kukwaza shughuli za kiuchumi, ndiyo lugha nyepesi unayoweza kuitumia kuakisi kiwango cha athari za mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini. Mvua hizo za El-Nino zilizoanza kunyesha Oktoba mwaka jana, hadi sasa zimefululiza kwa miezi saba na kukatisha uhai wa watu 162 nchini,…