
KONA YA MAUKI: Je, una kiu na ndoa yenye mafanikio?
Somo hili ni kwa ajili ya watu wenye ndoto ya kuwa na ndoa zenye mafanikio. Kama huna mpango wa kufunga ndoa hili somo si kwa ajili yako. Watu wengi wamekuwa wakifundishwa na kuelewa kwamba tunachotakiwa kuwa nacho ili tuishi kwenye ndoa ni upendo peke yake, upendo ukiwepo basi hakuna haja ya kingine chochote, mengine yatakuja…