
DC Timbuka: Tunapanga namna nzuri ya kuwanusuru wananchi na mafuriko
Siha. Kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kuathiri maeneo mengi nchini, Mkuu wa Wilaya ya Siha Mkoani Kilimanjaro, Dk Christopher Timbuka amesema wanapanga namna nzuri ya kuwanusuru wananchi na hatari ya mafuriko. Hata hivyo, amesema wakati Serikali ikiendelea na mipango na mikakati yake, amewomba wananchi nao waendelee kuchukua tahadhari hasa wale wanaoishi katika maeneo hatarishi…