
Hizi hapa dalili za changamoto ya afya ya akili kwa mjamzito
Mwanza. Kukosa usingizi wakati wa ujauzito, kujilaumu, kuwaza sana, kula sana na wakati mwingine kutokula kabisa ni miongoni mwa mambo yanayotajwa kuwa dalili za changamoto ya afya ya akili kwa mjamzito. Dalili hizo zimebainishwa leo Ijumaa Aprili 19, 2024 wakati wa kufunga mafunzo kuhusu changamoto ya afya ya akili kwa wajawazito na kina mama waliojifungua…