
Eti tusiwachape watoto wakikosea, tuwafanyeje?
Dar es Salaam. Mwaka jana nilipata bahati ya kutembelea sehemu zaidi ya tatu ambazo wazazi na walezi hawaruhusiwi kupiga watoto wao viboko. Na ninaposema hawaruhusiwi namaanisha hawaruhusiwi kwelikweli, sio ile ya tangazo tu, kwamba inakuja serikali au uongozi unatangaza kuwa hauruhisiwi kumchapa viboko mtoto, kisha wakimaliza kutangaza na kuondoka huku nyuma wazazi wanaweza kuendelea kuwacharaza…