Takukuru Geita yabaini kasoro kwenye miradi 1,800
Geita. Miradi 1,800 yenye thamani ya Sh7 bilioni iliyofuatiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Geita mwaka 2022/23 imebainika kuwa na kasoro zikiwamo za usanifu, ununuzi na baadhi ya fedha za miradi kuhamishiwa kwenye matumizi yasiyohusiana na mradi husika. Hayo yamebainishwa leo Aprili 18, 2024 kwenye kongamano maalumu linaloendelea mjini Geita…