Gereza la Kibondo lageukia ubunifu nishati safi ya kupikia
Kigoma. Jeshi la Magereza wilayani Kibondo mkoani Kigoma limeanza kutumia mkaa mbadala unaotokana na mchanganyiko wa randa za miti na udongo unaozalishwa ndani ya gereza hilo, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Serikali la matumizi ya nishati safi ya kupikia. Serikali, kupitia Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia (2024–2034),…