Ile ishu ya uwanja Yanga, kazi inaanza upya
KAMA ulidhani Yanga inapiga porojo katika ujenzi wa Uwanja pale Jangwani, tulia kwanza, kwani kuna mambo mazito yameshaanza na habari mpya ni rasmi mchakato wa kuongezewa eneo unakamilika leo Septemba Mosi. Kuanzia kesho Jumanne (Septemba 2), Yanga itakuwa inamiliki eneo la mita za mraba 37,500 pale Jangwani ikiwa ni baada ya kukamilisha eneo ambalo waliliomba…