
Haaland aipeleka Namungo fainali Tanzanite Pre-Season International
MABAO mawili yaliyofungwa na mshambuliaji wa Namungo, Abdulaziz Shahame ‘Haaland’ katika kila kipindi, yameifanya timu hiyo kufuzu fainali ya mashindano ya Tanzanite Pre-Season International. Namungo imeiondosha Tabora United kwa kichapo cha mabao 2-1, katika mchezo wa nusu fainali ya mashindano hayo uliochezwa leo Septemba 6, 2025 kwenye Uwanja wa Tanzanite Kwaraa uliopo Babati mkoani Manyara….