PATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO JUNI 27,2024
Home » PATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO JUNI 27,2024 Featured • Magazeti About the author
Home » PATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO JUNI 27,2024 Featured • Magazeti About the author
Arusha. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema hali ya uchumi nchini inazidi kuwa mbaya na watu wengi wakipitia ugumu wa maisha. Kimesema wakulima wanakabiliwa na changamoto za kupanda kwa gharama za pembejeo na soko la mazao yao kutokuwa na bei nzuri, huku wanakutana wakikabiliwa na ukosefu wa malisho na huduma za mifugo kuwa ghali….
*Asikiliza changamoto za wadau wa madini *Kliniki ya Madini kuanza Julai 3, 2024 *FEMATA watakiwa kuwa mabalozi na mfano katika kupambana na utoroshaji wa madini SERIKALI kupitia Wizara ya Madini imepiga marufuku Halmashauri kutoza tozo kwa Wachimbaji ambazo zipo kinyume na Sheria mama huku kliniki ya kutibu changamoto za wachimbaji wa madini ikipangwa kuanza Julai…
Dar/Mikoani. Saa 53 za mgomo wa wafanyabiashara ulioanza eneo la Kariakoo Dar es Salaam kabla ya kusambaa maeneo kadhaa nchini umeathiri mapato ya kada tofauti katika mnyororo wa biashara. Mgomo huo ulioanza alfajiri ya Jumatatu Juni 24, eneo la Kariakoo, hadi jana ulisambaa katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Mbeya, Mwanza, Iringa, Dodoma, Arusha,…
Arusha. Serikali kupitia Bohari Kuu ya Dawa (MSD) imetoa vifaa tiba na dawa zenye thamani ya Sh100 milioni kwa ajili ya kambi ya madaktari bingwa na wabobezi, inayoendelea jijini Arusha. Aidha, kutokana na wingi wa wagonjwa waliojitokeza, madaktari na wataalamu wa afya 100 wanatarajiwa kuwasili jijini hapa kuungana na wengine 450 ambao wanaendelea kutoa huduma…
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) imeanza kutekeleza kazi ya uchimbaji visima katika eneo la Mbezi- Msumi Kata ya Mbezi ikiwa ni maagizo ya Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Kundo Mathew katika ziara yake aliyoifanya mkoan Dar es salaam katika Wilaya ya Ubungo hivi karibuni. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea). Katika…
Mbeya. Athari ya mgomo wa wafanyabiashara wa maduka jijini Mbeya imeanza kuonekana kwa wananchi kuabza kulalamikia bei ya bidhaa kupanda. Inaelezwa vifaa na bidhaa zilizopanda bei ghafla ni vifaa vya shule ambavyo sasa wazazi wananunulia watoto wao kutokana na msimu za likizo kueleka kumalizika. Shule mbalimbali na msingi na sekondaro zinatarajiwa kufunguliwa kuanzia Julai mosi,…
Sengerema. Halmashuri ya Sengerema inapoteza zaidi ya Sh61milioini kila mwaka kutokana na kutokukamilika kwa ujenzi wa vibanda ya stendi kuu ya mabasi iliyoko Bukala mjini Sengerema kutokukamilika. Hiyo ni moja ya hoja tano zinazowasilishwa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwenye kikao cha baraza la madiwani la Halmashauri ya Sengerema. Diwani wa Tabaruka,…
Mufindi. Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Peter Serukamba, ameiagiza Halmashauri ya Wilaya Mufindi kuongeza nguvu katika usimamizi wa miradi ya maendeleo, ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati. Serukamba ametoa maagizo hayo leo Jumatano Juni 26, 2024 kwenye kikao cha Baraza la Madiwani lililojadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka…
Tarime. Baadhi ya wakunga wa jadi wilayani Tarime Mkoa wa Mara, wanadaiwa kuanza kujihusisha na vitendo vya ukeketaji wa watoto wachanga baada ya kuwazalisha wajawazito wanaokwenda kujifungulia kwao. Wakunga hao wanadaiwa kukeketa watoto wachanga baada ya baadhi ya mangariba kuacha kufanya shughuli hizo kutokana na kampeni mbalimbali zinazofanywa na serikali kwa kushirikiana na wadau wa mapambano…