Bado Watatu – 10 | Mwanaspoti
NIKAGEUKA na kumtazama mtu huyo aliyekuwa nyuma yangu na kumuuliza. “Ndiye yeye….amepatwa na nini sijui…?” “Inaonekana amejinyonga au amenyongwa.” “Ndiyo maana tangu jana sijamuona. Kumbe…!” Nikageuza uso tena na kuitazama ile maiti iliyokuwa inaning’inia. “Kama si wewe nisingetambua kama yeye ndiye Frank. Huyu jamaa anaishi na nani humu ndani?” “Anaishi peke yake. Aliwahi kuniambia kuwa…