Baraza lapitisha sheria kuidhinisha makisio ya matumizi ya fedha 2024/25
Unguja. Baraza la Wawakilishi limepitisha sheria kuidhinisha makisio ya matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2024/25. Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Saada Mkuya amesema kupitishwa kwa muswada huo kutaiwezesha Serikali kukopa fedha ndani na nje ya nchi, kwa ajili ya matumizi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Muswada una vifungu vinane kikiwemo kinachozungumzia…