JIWE LA SIKU: VAR sawa ije lakini kwenye viwanja vipi?
KWA mujibu wa Shirikisho la Kimataifa la Historia na Takwimu za Mpira wa Miguu (IFFHS), Ligi Kuu Tanzania Bara inashika namba sita kwa ubora barani Afrika nyuma ya vinara Misri, Morocco, Algeria, Tunisia na Afrika Kusini. Takwimu hizo zilitolewa Januari 2024. Ukiangalia orodha hiyo katika nne bora unazikuta nchi za Ukanda wa Kaskazini mwa Afrika…