TETESI ZA USAJILI BONGO: Kaseke ageuka lulu, Yanga na JKT kukutana mezani
FOUNTAIN GATE imeanza mazungumzo ya kumuongezea mkataba mpya nyota wa timu hiyo, Deus Kaseke aliye huru kwa sasa. Kaseke ameitumikia Fountain kwa miaka miwili tangu alipojiunga mwaka 2022 akitokea Yanga aliyodumau nayo kwa miaka saba tangu 2015 alipotokea Mbeya City, huku viongozi wakiamini bado ana uwezo mkubwa wa kuwasaidia msimu ujao. YANGA Princess imedaiwa kurudi…