Viongozi wa nchi za G7 wakubaliana kuipa msaada Ukraine – DW – 13.06.2024
Kwa mwaka wa pili mfulilizo, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy atahudhuria mkutano huo, akishiriki katika mazungumzo hayo leo Alhamisi. Rais Zelensky amesema anatarajia “maamuzi muhimu” katika mkutano huo ambapo pia atatia saini makubaliano ya usalama na Japan na Marekani. Viongozi wa G7 wanatarajia kutangaza angalau kimsingi mpango wa kuipa Ukraine mkopo wa dola bilioni 50 …