Admin

Raizin ataka 10 zaidi Bara

MSHAMBULIAJI wa Mtibwa Sugar, Raizin Hafidh amesema malengo aliyojiwekea msimu huu katika kikosi hicho ni kufunga zaidi ya mabao 10, huku akidai endapo atatimiza hayo itakuwa ni njia nzuri kwake kuwa na mwendelezo mzuri. Mshambuliaji huyo ambaye alikuwa sehemu ya kuirudisha Mtibwa Sugar katika Ligi Kuu Bara alimaliza Championship akiwa kinara wa upachikaji wa mabao…

Read More

Kipa aliyevunjika taya aanza mazoezi mepesi

KIPA wa Tabora United, Fikirini Bakari amerejea uwanjani baada ya kuwa nje akijiuguza kutokana na kudaiwa kuvunjika taya wakati akikiwasha katika mechi ya kirafiki dhidi ya Yanga iliyowafunga mabao 4-0 wiki iliyopita katika Uwanja wa  Gymkhana jijini Dar es Salaam. Fikirini alisema daktari alimwambia afanye mazoezi mepesi ya kukimbia na kuepuka kukongana na watu, na…

Read More

Bado Watatu – 20 | Mwanaspoti

ALINIPENDA sana na mimi nilimpenda. Alikuwa mwaminifu kwangu na mimi nilikuwa mwaminifu kwake. Alikuwa akisafiri kwa wiki mbili au tatu na kuniacha. Sikuwa na ushawishi wowote wa mwanaume na niliamini huko alikokwenda na yeye hakushawishika na wasichana.Miongoni mwa marafiki zake Sufiani ambao alikuwa akifika nao pale nyumbani alikuwa jamaa mmoja aliyekuwa akiitwa Shefa. Shefa alikuwa…

Read More

Hekaya za Mlevi: Zishtukieni sera za ndoto 

Dar es Salaam. Mimi sijui nina uraibu gani. Hata akipita mwendawazimu anayeongea peke yake, nitahangaika hadi nisikie kile anachosema. Mara kadhaa nimekuwa nikiwasikiliza paka wanaolalama usiku wa manane, nikawa nasikia kama wanaongea kama watu. Wakati mwingine niliogopa kwa kudhani nagombaniwa miye, maana mmoja alisema “ni wanguuu” mwingine akajibu “mwongooo”.  Kwa kutaka kujua kila kitu, najikuta…

Read More

JIMBONI KWA CHONGOLO NI FULL VIBE WAKIMSURI MGOMBEA URAIS CCM DK.SAMIA SULUHU HASSAN

Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Makambako  YAANI ni full vibe… ni shangwe tu kwa wananchi wa Makambako!Ndivyo unavyoweza kueleza wakati mamia ya wananchi wakiwa wamejitokeza katika mkutano wa kampeni wa mgombea Urais wa CCM Dk.Samia Suluhu Hassan  Katika mkutano huo ambao unafanyika mapema asubuhi ya leo Septemba 6,2025 wakimsubiri mgombea Urais kupitia CCM Rais Dk.Samia Suluhu Hassan…

Read More

Katwila aachiwa msala Geita Gold

ALIYEKUWA Kocha wa Bigman, Zubery Katwila amejiunga na Geita Gold kwa mkataba wa mwaka mmoja baada ya dili lake la kwenda Coastal Union ya Tanga iliyofanya mazungumzo naye mwanzoni ya kumhitaji kuingia dosari. Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa timu hiyo zimelidokeza Mwanaspoti kuwa Katwila amesaini mkataba wa mwaka mmoja na muda wowote kuanzia sasa…

Read More

Melo alaani ofisi za JamiiForums kuvamiwa, Msigwa amjibu

Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Jamii Forums, Maxence Melo amesema kuna uvamizi usio rafiki umefanyika katika ofisi zao zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam na amedai kuwa wavamizi walikuwa wakimtafuta yeye, huku Serikali ikisema haukuwa uvamizi bali ni utaratibu wa kawaida wa mawasiliano na anatakiwa kutoa ushirikiano na asizue taharuki katika jamii. Kupitia mtandao wake…

Read More

Chama aanza vitu Singida Black Stars

NYOTA mpya wa Singida Black Stars, Clatous Chama ameanza vitu na kuibua matumaini kwa kocha wa timu hiyo, Miguel Gamondi ambaye alikosa huduma yake katika mechi ya kwanza ya mashindano ya Kombe la Kagame dhidi ya Ethiopian Coffee kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo. Baada ya mechi hiyo, Gamondi alieleza wazi kwamba walikosa mtu mwenye…

Read More

Oviedo, Coastal Union kuna kitu kinapikwa

UONGOZI wa Coastal Union uko katika mazungumzo ya kumsajili aliyekuwa beki wa Pamba Jiji, Ally Ramadhan ‘Oviedo’ baada ya nyota huyo kumaliza mkataba, huku kukiwa hakuna mazungumzo ya kuongeza mwingine mpya wa kukichezea tena kikosi hicho. Nyota huyo wa zamani wa Mashujaa ameshindwa kufikia makubaliano ya kusaini mkataba mpya na Pamba ambapo kwa sasa inadaiwa…

Read More

Maajabu ya Kundi C Kagame Cup 2025

MICHUANO ya Kombe la Kagame imeanza kwa kasi, lakini tofauti na makundi mengine, Kundi C limeonekana kuwa la kipekee baada ya timu zote nne kuanza kwa sare katika mechi za kwanza. Katika mechi ya mapema iliyochezwa juzi Alhamisi, Kator ya Sudan Kusini ililazimishwa suluhu na Al-Ahly Wad Madani ya Sudan, kabla ya Al-Hilal Omdurman kutoka…

Read More