Mwenyekiti wa kijiji apigwa butwaa ‘wajanja’ kubandika stempu feki za TRA
Arusha. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Arusha imekamata kiwanda bubu kilichokuwa kinatengeneza pombe kali kinyume na sheria ambazo pia zinadaiwa kuwa na stempu za kodi za kughushi, huku mwenyekiti wa kijiji akibaki na mshangao. Kwa mujibu wa ukaguzi wa awali uliofanywa na maofisa wa mamlaka hiyo, stempu nyingine zimekutwa kwenye kiwanda bubu hicho…