Bado Watatu – 3 | Mwanaspoti
““HUMU ndani asiingie mtu yeyote. Tutarudi tena. Sawa?” “Humu ndani mnaishi watu wangapi?” “Ukiacha marehemu ambaye hakuwa na mke wala watoto, tuko familia tatu.” “Mwenye nyumba anaishi hapa hapa?” “Mwenye nyumba hakai hapa.” Nikatoka katika kile chumba pamoja na yule mtu. Polisi walikuwa wametangulia kutoka. Nikamuamrisha yule mtu afunge ule mlango. “Hakikisha hakuna mtu anayeingia…