Waziri Mkuu kuongoza majaribio SGR Dar-Dodoma Aprili 21
Dar es Salaam. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajiwa kuongoza safari ya majaribio ya treni ya reli ya kisasa (SGR) itakayofanya safari kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma ikiwa na watu takriban 600. Majaribio hayo yatafanyika Aprili 21, 2024. Katika treni hiyo Majaliwa ataambatana na viongozi wa Serikali, dini na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenda Dodoma…