Dk Nchimbi awaonya wanaCCM udalali kwa wasaka uongozi
Njombe. Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Emmanuel Nchimbi amewataka wanachama na viongozi wa chama hicho kujiepusha kuwa madalali wa watu wanaosaka nafasi za uongozi. Dk Nchimbi amesema kama kuna kitu kinachoweza kukidhoofisha chama hicho tawala ni viongozi kukubali kuwa madalali wa wagombea. “Mtu anayetaka kukufanya uwe dalali tafsiri yake ameshakupima, amegundua unanunulika,…