KIWANDA CHA KUONGEZA THAMANI GRAPHITE MBIONI KUJENGWA MTWARA.
Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa amesema kuwa Kampuni ya Volt Graphite Tanzania Limited (VGT) ipo katika majadiliano ya mwisho na wanunuzi wa Madini ya Kinywe (Graphite) ili kuruhusu kuanza kwa ujenzi wa kiwanda cha kuongeza thamani ya madini hayo Wilayani Masasi, Mkoa wa Mtwara. Ameyasema hayo leo Juni 07, 2024, Bungeni, Jijini Dodoma…