Mafuriko yafunga shule nne Kyela, Sh35 milioni kusaidia waathirika
Mbeya. Serikali imezifunga shule nne zilizoko katika Kata ya Katumba Songwe wilayani Kyela Mkoa wa Mbeya kutokana na kuzingirwa na maji ya mafuriko. Maji hayo mpaka sasa yamezingira pia makazi ya watu na leo Jumamosi Aprili 20, 2024 Serikali imepeleka msaada wa fedha taslimu Sh35 milioni zitakazowasaidia waathirika. Mafuriko hayo yaliyoanza Machi, mwaka huu, …