TPC na mipango ya kuwainua wanawake gofu
KATIKA kuhakikisha usawa wa kijinsia kwenye mchezo wa gofu, klabu ya TPC Moshi imeanza rasmi mchakato wa kuongeza idadi ya wachezaji wa kike. Mzuka wa gofu, kupitia gazeti la Mwanaspoti limefanya mahojiano na nahodha wa TPC, Jafari Ali ambaye anataja mipango ya klabu hiyo. Anasema mkakati wa klabu hiyo ni kuhakikisha wanawapata wanachama wa kike…