Mama asimulia watu wasiojulikana walivyompora mwanawe mwenye ualbino
Muleba. Mkazi wa Kitongoji cha Mbale, Kijiji cha Bulamula wilayani Muleba mkoani Kagera, Judith Richard (20) amesimulia jinsi watu wasiojulikana walivyompora mtoto wake mwenye ualbino na kutokomea naye kusikojulikana. Tukio la mtoto huyo wa kike, Asimwe Novath (2) kukwapuliwa mikononi mwa mama yake, lilitokea Alhamisi Mei 30, 2024, saa 1 jioni na msako wa kumtafuta…