PATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO MEI 28,2024
Home » PATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO MEI 28,2024 Featured • Magazeti About the author
Home » PATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO MEI 28,2024 Featured • Magazeti About the author
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam May 28, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za nyuma za Magazeti ya Tanzania. The post Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo May 28, 2024 first appeared on Millard Ayo.
Unguja. Zanzibar imesajili laini za simu za mezani na mkononi 849,082 sawa na kadirio la watumiaji 446,885. Kati ya laini hizo, idadi ya watumiaji wa simu za mkononi ni 439,470 na simu za mezani ni 7,415 ambao ni sawa na asilimia 23.6 na asilimia 0.4 ya wakazi wa Zanzibar. Kwa mujibu wa sensa ya watu na…
Moshi. Siku tatu baada ya kutokea kifo cha Ephagro Msele (43) anayedaiwa kuuawa kwa kuchomwa kisu na mkewe Beatrice Elias (36), Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro limewakabidhi ndugu mwili wa marehemu. Kwa mujibu wa Polisi, tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Mei 25, 2024 saa 3:50 usiku katika Kitongoji cha Pumuani A, Kata ya…
Dar/Mikoani. Kama umewahi kuhisi maumivu ya kutwishwa mzigo mzito zaidi ya nguvu zako, basi hali hiyo ndiyo inayoukabili Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa), katika jukumu la uendeshaji wa vivuko nchini. Temesa inatekeleza jukumu hilo kwa mujibu wa sheria ya kuanzishwa kwake ya mwaka 2005, inayotaka pamoja na majukumu mengine ya msingi, wakala huo uwajibike…
Dodoma. Unaweza kusema kuti la mazoea limemuangusha mgema, msemo unaoendana na kile kinachowakuta wabunge, manaibu waziri na mawaziri kupigwa viwanja na wajanja. Pengine walijua wanaopigwa ni wanyonge peke yao na kuchelea kuwabaini na kuwakomesha wachache waliokuwa na tabia hiyo, wamekubuhu sasa wanawatapeli hadi watunga sheria wa nchi. Hali hiyo imemsukuma Waziri wa Ardhi, Nyumba na…
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema Maadhimisho ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu ni sehemu ya mikakati ya serikali katika kuongeza hamasa ya kukuza elimu ujuzi na ubunifu katika kuchangiza maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Mkenda amesema hayo Mei 27, 2024 jijini Tanga wakati akifungua Maadhimisho hayo ambapo amesema…
SPIKA wa Bunge, Dkt. Tulia Akson ameisisitiza Wizara ya Ujenzi kupitia Wakala ya Barabara (TANROADS) kuhakikisha miradi yote ya barabara inayokamilia inapimwa ubora kwa kutumia vifaa maalum kabla ya Makandarasi kuikabidhi kwa serikali. Dkt Tulia amesema hayo leo tarehe 27 Mei 2024 Bungeni Jijini Dodoma wakati akifungua Maonesho ya siku mbili ya sekta ya Ujenzi…
Dar es Salaam. ’Inawezekanaje zaidi ya wanafunzi 600 wa shule moja kulewa na kulala darasani wakati wa masomo? Swali hili limekuja ikiwa ni siku chache baada ya Mbunge wa Kibamba, Issa Mtemvu kudai kuwapo kwa tatizo kubwa la maadili ya watoto ndani ya jimbo lake. “Katika Jimbo la Kibamba ambako Rais amejenga shule nzuri kwa…
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Daniel Chongolo amechangia Tsh Milioni 5 wakati akiongoza Harambee katika Kanisa la Waadventista Wasabato katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Tarehe 26 Mei, 2024 ambapo zaidi ya Milioni 47 na mifuko 460 ya saruji imepatikana kuwezesha ujenzi wa Kanisa hilo.