Miili minne yapatikana ajali ya mtumbwi Katavi
Katavi. Miili ya watu wanne kati ya saba wanaohofiwa kufariki dunia kwa ajali ya mtumbwi katika Mto Lunguya uliopo Kitongoji cha Lunguya Kijiji cha Mwamapuli mkoani Katavi imepatikana. Mtumbwi huo uliokuwa umebeba watu 14 na mizigo ya mazao ulipinduka Mei 26, 2024 ukidaiwa kuzidiwa na uzito na watu saba kuzama majini. Akizungumza na Mwananchi leo…