Lissu: Ugumu wa maisha utamalizika tukipata Katiba mpya
Dar es Salaam. Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)-Bara, Tundu Lisu amesema suluhisho la kumaliza ugumu wa maisha uliotamalaki nchini Tanzania ni kwa wananchi wakubali kuanza kutafuta Katiba Mpya. Amesema ugumu huo unachangiwa na upungufu wa Katiba iliyopo kiasi kwamba imezalisha utawala wa viongozi wenye miungu wengi wanaopanga maisha ya watu badala…