Wanawake wanufaika wa Tasaf wafungua kiwanda cha kusaga karanga
Mwanza. Wanawake 15 wa kikundi cha Wasikivu katika Mtaa wa Kabangaja, Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, wameazisha kiwanda kidogo cha kukaanga na kusaga karanga pamoja na kutengeneza sabuni, baada ya kuwezeshwa mtaji wa Sh11.5 milioni kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (Tasaf). Kikundi hicho, chenye wanachama wote wanawake na walengwa wa mpango huo, kilianzishwa mwaka…