Thiago Silva kama kawa amemalizia hisani nyumbani
YUKO wapi yule aliyesema hisani inaanzia nyumbani? Wazungu huwa wanaandika kwa Kiingereza chao kizuri ‘charity begins at home’. Ni kweli. Lakini Wabrazil nao wangeweza kuendeleza sentensi hiyo na kuandika ‘hisani pia inaishia nyumbani’. Wiki ile nyingine nilimuona Mbrazili Thiago akilia katika viunga vya uwanja wa mazoezi wa Chelsea, Cobham. Labda ana hisia kali na Chelsea…